Sunday, 16 October 2016

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOKUWA NYUMBANI KWA AJILI YA USALAMA WAKO.

  1. Badili au fanya matengenezo kwenye kifaa cha umeme kilichoharibika au kulegea kwa namna yoyote.
  2. Usipitishe extension cable katika milango au chini ya zuria(carpet).
  3. Katika nyumba yenye mtoto/watoto wadogo hakikisha vifaa vyote vya umeme ni vile visivyoweza kung'oka, kunyofoka ama kuhamishika kwa urahisi.
  4. Unaweza kuongeza switch za ukutani(switch socket) nyingine ikiwa una uhitaji huo badala ya kutumia extension cable.
  5. Fuata maelekezo ya mtengenezaji kila mara unapotumia kifaa chochote cha umeme.
  6. Epuka kuunganisha vifaa vingi vinavyotumia umeme katika switch ya ukutani(switch socket) moja au extension cable moja.
  7. Ikiwa switch za ukutani au za taa zinapata joto, au fuse kuungua mara kwa mara na wakati mwingine taa kupunguza mwanga  au kuwaka na kuzima, mtafute haraka mtaalam wa umeme anayetambulika kisheria.
  8. Hakikisha nyumba yako ina vifaa vyote vya ulinzi katika mifumo ya umeme ya nyumba yako vinavyohitajika. Vijaribu mara kwa mara ikiwa vinafanya kazi kwa ufanisi.
Haya ni baadhi tu kati ya mengi. Ni vizuri tukajenga tabia ya kufuata maelekezo na miongozo ya wataalam waliotengeneza vifaa tunavyovitumia au hata wale wenye taaluma ya mambo haya ili kuepuka majanga yanayoepukika.
Previous Post
Next Post

About Author

0 comments: