Thursday, 6 October 2016

UMEME JUA (SOLAR POWER)

Image result for solar panel images


Huu ni umeme unaozalishwa kutokana na mionzi kutoka katika jua. Ili mionzi hii ibadilishwe kuwa katka nguvu ya umeme kuna hatua kadhaa hufanyika. Hata hivyo kuna muunganiko wa idadi fulani ya vifaa ambao hukamilisha mfumo mzima wa umeme jua. Kutokana na maelezo haya, utahitaji vifaa vifuatavyo ili kuzalisha umeme huu;

  1. Solar Panels
  2. Charge Controller
  3. Power Inverter
  4. Batteries
  5. Surge Arrestor
Baada ya kujua vifaa utakavyohitaji, utatakiwa kufanya mahesabu ya idadi na ukubwa wa solar panels na batteries utakazohitaji ili kufanikisha zoezi hili. Pia utahitaji kujua aina ya muungano wa batteries zako pamoja na ukubwa wa nyaya utakazotumia. Leo nitakuchambulia kwa kifupi kila kifaa nilichokitaja hapo juu.

Solar Panels. Kazi ya solar panel ni kubadilisha nguvu ya mionzi jua kuwa nguvu ya umeme na hivyo kuzalisha umeme kwa ajili ya kuchaji batteries.

Charge Controller. Kazi yake kubwa ni kuilinda battery. Huhakikisha battery inachajiwa kwa usahihi katika kiwango kinacholingana na uwezo na ukubwa wa battery yenyewe. Hali hii huisaidia battery kudumu kwa muda mrefu.

Power Inverter. Kifaa hiki ni moyo wa mfumo huu wa umeme jua. Kazi yake ni kubadilisha 12V DC ambao ni umeme wa battery kuwa 220V AC ambao ndio umeme wa matumizi majumbani mwetu. Inverter ina uwezo wa kuchaji bettery pia ikiwa itaunganishwa kwenye jenereta au umeme wa TANESCO. 

Surge Arrestor. Radi inaweza kusababisha uharibifu mkubwa sana kwnye mfumo mzima wa umeme jua. Janga hili linaweza kupunguzwa kama sio kumalizwa kabisa kwa kuunganisha surge arrestor katika mfumo wa umeme jua wako.

Storage Battery. Mara zote ni 12V DC battery. Zinatunza umeme katika hali ya kikemikali. Bila umeme unaozalishwa na solar panel kutunzwa, maana yake ni kwamba utapata umeme pale tu jua linapokuwepo.

Kesho nitakueleza namna ya kufanya mahesabu ili kujua ni solar panels na batteries ngapi utahitaji kutokana na matumizi yako. Ni mahesabu rahisi ambayo yeyote anaweza akamudu kuyafanya.


Image result for solar panel images

About Author

Related Posts

0 comments: