
Ni ukweli ulio wazi kabisa kwamba wengi wetu hatufahamu AVR ni nini. Kwa sababu hiyo hata umuhimu wa kifaa hiki haufahamiki. Kwa wale wanaojua umuhimu wake ni kawaida kabisa kuona zaidi ya AVR moja katika nyumba ama ofisi zao. Kwa sababu ya umuhimu wake sio ajabu kuona AVR sebuleni, chumbani au jikoni ikihudumia vifaa vinavyohitaji huduma yake.
Hata hivyo si vifaa vyote vya majumbani au ofisini vinahitaji kuunganishwa na AVR. Mfano wa vifaa hivyo ni feni, blower, jiko la umeme, pasi, n.k. Najua una shauku ya kujua ni vifaa gani vitahitaji kuunganishwa na AVR na kwamba kwa nini vifaa hivyo viunganishwe na kifaa hiki muhimu. Nitakutajia vifaa baadhi kama TV set, computer, jokofu(fridge), kingamuzi, music system, n.k. Ni muhimu vifaa hivi vikaunganishwa na AVR kutokana na unyeti na urahisi wa kuathiriwa kwa mifumo yake kunapotokea kiasi cha umeme kisichokubalika kuingia katika mifumo yake.
Automatic Voltage Regulator (AVR) ni kifaa chenye mchanganyiko wa umeme na mifumo ya kielektroniki kinachofanya kazi ya kuhakikisha umeme unaotoka kuelekea kwenye chombo chako cha umeme unakuwa wa uhakika na katika kiwango sahihi kinachotakiwa. AVR zinapatikana katika ukubwa tofauti tofauti. Ninaposema ukubwa namaanisha uwezo wake wa kupokea na kutoa kiasi cha umeme unaohitajika. Kwa hiyo maana yake ni kwamba kabla ya kununua AVR yako ni muhimu sana kujua idadi na kiasi cha umeme ya kila kifaa chako unachokusudia kukiunganisha kwenye AVR. Uwezo wa AVR unapimwa na kipimo ambacho kitaalamu kinaitwa VA. Kwa hiyo kuna AVR za ukubwa wa 500VA, 1000VA, 1500VA, 2000VA, 3000VA, 5000VA. VA ni matokeo ya Voltage x Ampere. Kwa wale waliofanikiwa kusom Physics kidogo wataelewa kwamba VA inamaanisha Power, ingawa katika umeme kuna aina nyingi za power. Sijakusudia kuongelea power ila nilitaka ujue kwamba hizo tarakimu hapo juu zinawakilisha Power (Nguvu/uwezo wa umeme).
Ni muhimu sana kutumia AVR nyumbani au ofisini kwako kwa sababu umeme unaoingia katika majengo yetu ni wakati fulani unacheza cheza. Yaani unapanda na kushuka (unaongezeka na kupungua). Hali ya namna hii ya umeme inaweza kusababishwa na radi, mifumo mibovu au iliyochoka ya kudhibiti mwenendo wa umeme na wakati fulani uharibifu wa dharura wa mifumo ya kusafirisha umeme. Kumbuka nimesema wakati fulani, namaanisha si mara zote hali hii hutokea, ni mara chache sana. Sasa hali hii ya kupanda na kushuka kwa umeme inaweza kusababisha vifaa/vyombo vyako vya umeme kupata uharibifu kama sio kuviangamiza kabisa.
AVR ina mfumo mzuri ndani yake wa kukinga na kulinda vifaa vyako vya umeme wakati wote. Tatizo likiwa kubwa zaidi AVR inauzuia kabisa umeme kuingia katika kifaa chako. Hivyo ni bora kuingia gharama ya kuwa na AVR nyumbani au ofisini kwako.
Here is Mr Benjamin contact Email details, 247officedept@gmail.com. / Or Whatsapp +1 989-394-3740 that helped me with loan of 90,000.00 Euros to startup my business and I'm very grateful,It was really hard on me here trying to make a way as a single mother things hasn't be easy with me but with the help of Mr Benjamin put smile on my face as i watch my business growing stronger and expanding as well.I know you may be surprised why I put things like this here but I really have to express my gratitude so anyone seeking financial help or going through hardship with their business or want to start a business project can see this and have hope of getting out of the hardship..Thank You.
ReplyDelete