Saturday, 17 January 2026

Tozo za umeme kwa wapangaji

 


Je unafahamu kwamba wamiliki wa nyumba hawapaswi kutoza bei ya umeme kubwa zaidi kuliko TANESCO?

Kwa mujibu wa taarifa zinazopatikana kwenye tovuti ya shirika la umeme Tanzania (TANESCO), mwenye nyumba (Mpangishaji) haruhusiwi kumtoza gharama za umeme Mpangaji wake tofauti na bei elekezi zilizowekwa bayana na shirika hilo. Nanukuu taarifa hiyo;

"Wateja wanapaswa kulipa bei ile ile ambayo shirika linatoza,hakuna anaruhusiwa kuuza umeme bila kibali cha mamlaka zinazohusika.Aidha wateja wanashauriwa kuhakikisha maswala yote ya malipo ya umeme au endapo kutakuwa na deni yanaingizwe kwenye mkataba wa pango ili kuondoa sitofahamu ambayo inaweza kujitokeza baadaye" Mwisho wa kunukuu.

Nawakumbusha wenye nyumba na yeyote anayehusika, ni kosa kuuza umeme bila kibali halali kutoka mamlaka halali.

Latest
Next Post

About Author

0 comments: