
Wakati technolojia imesababisha vitu vingi kuwa rahisi maishani mwetu, kuchagua jokofu zuri miongoni mwa zaidi ya mamia ya aina za majokofu sio rahisi kama ambavyo wengi wanafikiri. Aina ya maisha na ukubwa au udogo wa familia ni baadhi ya mambo yanayoathiri aina ya jokofu unalotakiwa kuwa nalo.
- Hatua ya kwanza kabisa itakayoamua aina ya jokofu unalolitaka ni kiasi cha pesa ulichotenga au ulichonacho. Kama ilivyo kwa bidhaa zingine, majokofu yanapatikana katika bei tofauti tofauti kulingana na uzuri, ukubwa au udogo, ama hata kampuni iliyotengeneza jokofu hilo.
- Hatua ya pili ni kuangalia ni kiasi gani cha vyakula na vinywaji utahitaji kuhifadhi katika jokofu lako. Hapa namaanisha nafasi(au ukubwa) wa jokofu. Kitu muhimu ni ujazo wa jokofu hilo.
- Utahitaji kujua upana na urefu (width and height) wa jokofu unalotaka kununua. Kwa ujumla hata kama utahifadhi vyakula na vinywaji vingi(ikiwa tu ni kwa matumizi ya nyumbani) utahitaji jokofu lenye urefu na upana usiozidi 1.7m urefu na 0.9m upana yaani 170cm(68inches)urefu na 90cm(36inches). Jokofu lako jipya litahitaji kukaa vizuri katika jiko lako ama sehemu nyingine yoyote utakayoona inafaa. Hivyo kuwa makini unapopima ukubwa wake, bila kusahau kupima urefu na upana wa milango na njia litakapopitishwa jokofu wakati wa kuingia ndani.
- Chagua aina kadhaa tofauti tofauti za majokofu. Kila moja likiwa na faida/uzuri (pros) na hasara/ubaya(cons) wake. Angalia bei,aina na mwonekano wake. Tafakari mwenyewe ikiwa unahitaji jokofu la milango miwili au mmoja, au ikiwa unataka lile linalopooza upande wa chini na upande wa juu linagandisha kabisa na kinyume chake. Au wakati mwingine unataka linalopooza upande wa kushoto na kugandisha upande wa kulia.
- Angalia namna jokofu lilivyo kwa ndani. Chunguza kama lina vyumba ambavyo ni adjustable kwa maana ya kuweza kuongeza au kupunguza urefu wa vyumba vilivyomo(shelves that split) kulingana na mahitaji yako ya wakati husika. Majokofu mengine yana vyumba ndani yake visivyoweza kupunguza au kuongeza urefu (height) wake.
- Angalia aina ya jina la kampuni ambalo ikitokea limeharibika basi ni rahisi kupata mafundi na vipuli vyake kwa ajili ya matengenezo. Jaribu pia kuuliza kutoka kwa watu wengine unaowafahamu kuhusu aina ya jina la kampuni la jokofu unalotaka kununua ikiwa wana uelewa au wameshawahi kutumia au wanatumia aina ya jokofu unalolitaka.
Ni vizuri pia kutafuta ushauri wa kitaalam kutoka kutoka kwa mtaalam yeyote unayemwamini ambaye ana leseni inayotambuliwa na serikali. Ni muhimu sana kufanya hivyo kwani kuna mambo mengine mengi ya kitaalam yanayopaswa kuzingatiwa ambayo hayawezi kuandikwa humu na kila mtu akayaelewa.
0 comments: