Kabla ya kuendelea na mjadala wetu wa leo kuhusu vyanzo vya moto unaosababishwa na umeme, nataka ufahamu ukweli ufuatao;
- Mgunduzi Edson aligundua kiti cha umeme si kwa matumazi ya kunyongea isipokuwa kuuelezea ulimwengu hatari ya umeme ilivyo kubwa ikiwa kanuni za umeme hazitazingatiwa.
Hatimaye nataka tuangalie vyanzo vikubwa vya majanga ya moto hasa katika nchi yetu ya Tanzania. Sijafanikiwa kupata takwimu sahihi kutoka kikosi cha zimamoto, lakini kwa utafiti usio rasmi inaonesha vyanzo hivyo ni pamoja na;
- Mishumaa
- Umeme
- Uchomwaji wa majani mashambani kiholela
- Matumizi yasiyo sahihi ya mafuta ya taa, diesel, petrol na gas.
Hata hivyo lengo langu hapa ni kutaka kuonesha vyanzo baadhi vya majanga ya moto yanayotokana na umeme. Nataka kuweka angalizo muhimu kwa watumiaji wote wa umeme. Ni muhimu ukavifahamu vyanzo vichache vifuatavyo;
- Taa za umeme na vifungashio vyake.
- Heater za umeme
- Vifaa vyote vinavyotumia umeme.
- Switch za umeme za aina zote.
- Wiring ya umeme iliyofanywa bila kuzingatia viwango.
- Wiring ya umeme iliyochakaa.
- Maungio ya nyaya (junction) yaliyolegea.
- Kutumia kifaa chochote cha umeme kinachotumia umeme mkubwa kuliko uwezo wa waya uliofunga katika mfumo wako wa wiring.
- Vifaa vingine vya umeme kama transformer, pasi, motor, n.k.
Nia yangu ni kutaka kusisitiza kwa watumiaji wa umeme kufanya ukaguzi katika vitu nilivyovitaja hapo juu kila inapobidi. Wengi wetu hatuna utamaduni huu. Kama ningetaka kuuliza wangapi wamewahi kufanyia ukaguzi mifumo yao ya umeme majumbani mwao ama maofisi, pengine ningempata mmoja katika kila watu kumi. Tusisubiri majanga.
Sambamba na hilo wataalam wetu wa zimamoto wanatusisitiza kumiliki vifaa vya kuzimia moto(fire extinguishers) katika nyumba tunamoishi. Wataalam hawa wamefika mbali zaidi kwani wanasisitiza ramani zetu za nyumba kuzipitisha kwao kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kutekeleza ujenzi wake kama tunazozipitisha kwa wataalamu wengine yaani wahandisi wa ujenzi. Hii ni kwa ajili ya kushauri namna milango na madirisha au kijisehemu cha kutokea cha dharura itawekwa endapo kutatokea janga la moto.
Hata hivyo si kila kitu/kifaa kinachoweza kuzima moto unaweza kukitumia kuzima moto uliotokana na umeme. Kwa mfano maji, kamwe usijaribu kuzima moto wa umeme kwa kutumia maji. Hata fire extinguishers zipo za aina tofauti mfano zenye hewa ya carbon na zenye unga maalum. Unaweza kujua kwa urahisi ni ipi inafaa kwa kuzima moto wa umeme.




Educative, Nmeelimika sana
ReplyDeleteAsante
Delete